Tuesday 21 October 2014

MISS TZ 2014 SITTI MTEMVU, NI MISS HALALI MWENYE VIGEZO VYOTE!


Kamati ya Miss Tanzani imesema kuwa haiwezi kumvua taji Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kwa kuwa ni Miss halali na mwenye vigezo vyote vilivyotakiwa, na amewataka watu kutoropoka kwa kuwa hawajui vigezo vinavyotakiwa
Akifafanua kuhusu suala la umri, mratibu wa mashindano hayo Hashim Lundenga amesema kuwa cheti halali walichonacho wao ni kile kinachoonesha Sitti Mtemvu kazaliwa 24 mei 1991 na si vinginevyo.

Kuhusu suala la passport na leseni zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii zikionesha amezaliwa mwaka 1989, Lundenga amesema wao huwa hawangaali vitu hivyo wanachojali ni cheti cha kuzaliwa.

Kuhusu tuhuma za unene amesema wao huwa hawaangalii wembamba wala ufupi, muhimu ni awe na vigezo vinavyotakiwa
 
CREDIT:EAST AFRICA TV

1 comment:

  1. Jamani watanzania tuache ushabiki,Sitti ndie miss reds 2014 sasa huyo asiemtaka angekua yeye.Ndo hapo arudi na taji la Miss world sijui mtasema hastahili!!!!

    Watu Wa ajabu Sana nyie

    ReplyDelete